Utangulizi

Mnamo mwaka 1965 tulitoa kitabu chetu cha kwanza,  “Muongozo wa Ibada za Kiroho”.

Wakati huo kulikuwa kuna upungufu mkubwa katika soko la vitabu, katika suala hili... Ilikuwa lazima kitabu hicho kitolewe katika wakati ule ambapo vitabu vya dua visivyokidhi haja ndivyo vilikuwa vimejazana.

Kwa kadiri ya uwezo wetu tuliandaa kwa mtazamo uliozoeleka na kutoa kwa ajili ya matumizi ya ndugu zetu wapenzi wa kiislam, kitabu cha dua kidogo lakini chenye kujitosheleza

Sifahamu ni kiasi gani kitabu hiki kilichochapishwa kwa wingi kimesambaa Uturuki katika kipindi cha miaka mingi iliyopita katikati. Lakini, sintoweza kushukuru vya kutosha kwa kiasi nilivyoona na kusikia idadi ya watu na nyumba zenye kitabu hiki...

* * *

Katika utoto wangu baba yangu alilete nyumbani kitabu cha dua kinachoitwa “REHBERİ İBADÂTİL MANEVİYE” ... kama alivyokuwa mama yangu, kwa hamu na shahuku nilikisoma na kujaribu kunufaika nacho katika matatizo yangu mbalimbali. Mfano, nilikitumia kwa haja zangu na kujiongezea imani. Na bila shaka faida zake nimeziona... Nilipooa, baba yangu alininunulia kitabu kama hicho; na ninaendelea kukisoma mpaka sasa...

Hiyo ni mistari kutoka kwenye barua ya msomaji wetu ambaye ana watoto wakubwa tu hivi sasa.

Naam, Alhamdulillah, kitabu chetu kilipita kwa vizazi hadi vizazi; kimepata daraja ya “Kitabu cha enzi”.

Hata hivyo, katika kipindi cha katikati, kama matokeo ya utafiti wetu, na kwa ufunuo wa muumba tumefahamu taratibu nyingi zaidi. Na tumetaka kwa kadiri iwezekanavyo tugawane na idadi kubwa ya waislamu ujuzi huu wenye faida...

Kwa upande mwingine kinatakiwa kiwepo kitabu cha <<DUA na DHIKIRI>> ambacho kitajibu maswali kuhusu mada hizi mbili kwa mujibu wa elimu na ufahamu wa kizazi kinachokua.

Kitabu chetu cha kwanza, kutokana na uzoefu mdogo ulioambatana na ujana, tulikiacha chini ya udhibiti wa mchapishaji, kwa sababu ya kutoa haki ya usambazaji... Hivyo basi safari hii, kwa uwezo wa Allah, tunakitoa kama zawadi kwa ndugu zetu wote wa kiislamu. Kitabu chetu hiki hakina haki ya usambazaji! Hakikuandikwa kwa ajili ya pesa. Yeyote atakaye, kwa sharti la kuwiana na kitabu asili, anaweza kunufaika na kitabu hiki na pia kuwanufaisha wanaomzunguka... Anaweza kuwazawadia rafiki zake wa kiislamu. Itakuwa vizuri sana kama akituombea radhi sisi kwa kusema “Allah akuridhie” na kutusomea “Ihlas tatu na Fatiha moja”...

Rasulu wetu Muhammad Mustafa alayhi swalaatu wa sallaam, kiongozi wetu kasema , “Atakayesaidia jema, anakuwa kama amelifanya jema hilo”.

Naomba, Allah atufanye tuwe wenye kusaidia mema katika uhai wetu wote; Atupe hifadhi tusiwe vyombo vyenye kusababisha shari na kufanya matendo yatakayotujutisha kesho...

Allah atujaalie kunufaika na kitabu hiki, na atuwezeshe tuelewe thamani ya mali iliyopo mikononi mwetu.

Asili 

  

 

Matamshi: Laa ilaaha illallah 

Maana:

Kiswahili: Hukuna mungu, Allah Pekee

 
Kiingereza: There is no GOD, only ALLAH


Kituruki: Tanrı yok, sadece ALLAH var