Namna Ya Dua

Kuna baadhi ya matendo yenye umuhimu mkubwa unapofanya DUA...

Unapofanya dua, inabidi mikono uiweke mbele hali ya kuwa viganja vi sambamba na uso na imeachaniswa kwa pembeni kuacha makwapa wazi. Inakuwa yenye matokeo mazuri viganja vikiwa katika umbali wa kama sentimeta 30 kutoka usoni hali ya kuwa kuna uwazi kati ya vidole ili mionzi inayotoka katika kipaji cha uso iungane mbele na ile itokayo katika vidole.

Tazama Rasulu Alayhi swalaatu wasalaam anasema nini kuhusu hili:

“Mja yeyote akinyanyua mikono yake hali ya kuwa makwapa yanaonekana na kuomba kwa ALLAH; dua yake itajibiwa kama hatokuwa ni mwenye kuharakisha.

- Haraka inakuwa aje ya Rasulallah?..

- Usema , nimefanya dua lakini haijakubaliwa” (Anaachana nayo)... hili ni kosa; Inabidi kuendelea mpaka dua itakapo fanikiwa.

Mionzi itokayo kwenye ncha za vidole na mionzi yenye uelekeo maalumu itokayo kwenye ubongo ni yenye umuhimu mkubwa katika kufanikisha jambo pale inapoungana na kufanya athari za namna ya mionzi ya LAZER.(Zaidi katika vitabu vyetu vya “Mtu na siri zake” na ”Utazamaji wa Mpweke”).

Kama inavyobainika hapa, nguvu mama inayopelekea ufanikiwaji wa dua, si yenye kuja kwa mtu kutoka nje; bali ni yenye kuzaliwa kutoka kwenye nguvu ya kiroho ya majina ya Allah yaliyopo katika uwepoji wa mtu.

Kwa kifupi DUA ni zoezi lifanywalo na mtu la kufanikisha matakwa yake kwa kutegemea nguvu za kiungu zilizo ndani yake.

Msingi wa DUA ni “Mawimbi yenye uelekeo maalumu...

Kama ambavyo utokeaji wa awali wa ulimwengu ni udhihirikaji wa fikira ya Allah kwa badiliko kutoka ukanda(dimension) wa elimu kuwa nguvu(energy) na umbile la kikwanta, hata matakwa na matamanio ya mtu yanatokea katika namna ya mkusanyiko, kwa msaada wa mawimbi ya ubongo yenye uelekeo maalumu, wa matakwa na matamanio ya ufahamu yatokayo katika ukanda(dimension) wa elimu.

Ni kwa sababu hii basi jinsi daraja la kuyakusanya mawazo(concentration) linavyoongezeka ndivyo hivyo hivyo majibu ya dua yanavyopata kasi. Ndiyo maana imesemwa kwamba, “Dua ya aliyedhulumiwa haipotei; hapati faraja aliyepokea ah! (aliyenung’unukiwa) !..”

Kwani, mtu anayefanya “ah”, kwa machungu aifanyayo nayo; kwa mkusanyiko wa mawazo aifanyayo nayo anaelekeza mawimbi negativu ya ubongo kwa huyo mtu katika namna ya kwamba, inakuwa haiwezekani hata kidogo mtu huyo kuukwepa mshale wa mawimbi hayo...

Matokeo ya hiyo “ah”  kama hayakutokea kwa babu basi yatatokea kwa mjukuu!.. Ki vipi? Rahisi tu!..

Mawimbi ya Ah aliyoyapata babu, jinsi yanavyoathiri mfumo wake wa jenetikia, hata kama matokeo yake hayatodhihirika kwake, yatadhihirika kwa mtoto wake au mjukuu wake kutokana na mpokezano wa jeni; na anakumbwa na adhabu ya babu yake. Ni kwa sababu hii ikasemwa, “Babu kaiba tunda, meno ya mjukuu yemechomoka”.

Naam! Tumesema viganja viwe mbele, mikono iwe imeachana katika dua... Kiongozi wetu alifanya hivyo.

Hazrat Rasulullah pamoja na maswahaba walifanya dua hali ya kuwa wamesimama na viganja vyao vimenyanyuliwa kama tulivyoeleza,  dhidi ya wale waliotoweka baada ya kuwauwa watu waliowakuta wenyewe jangwani wamejeruhiwa na kuwasafisha majereha na kuwaponyesha; Watu hao walipatikana baada ya muda mfupi sana na kupata malipo ya walilofanya.

Kama ilivyo kwa dua ifanywayo kwa namna ya mawimbi “yenye uelekeo maalumu” kwa msaada wa ncha za vidole hali ya kuwa umesimama na viganja vipo kama tulivyoeleza vikitazama uso na mikono imelala kwa mbele, dua inayofanywa katika hali ya kusujudu pia ina athari kubwa sana.

Hasa dua inayofanywa katika SIJIDA baada ya nusu ya usiku, yani muda ambapo jua lipo nyuma ya mahali ulipo na mionzi ya jua iko katika nguvu ya chini kabisa, ni yenye athari ya daraja la juu sana. Kama dua hii itafanywa katika sijida ya mwisho ya swala ya haja au swala nyingine yeyote nguvu ya athari inakuwa kubwa zaidi...

Kama dua itafanywa katika sijida ya mwisho ya swala, yani swala ya usiku, baada ya kukiri mapungufu ya aina mbalimbali na kuomba kusamehewa kutegemeana na kitu kinachohitajika, kama utaendelezwa utaratibu huu kwa siku kadhaa bila kuacha au katika namna ya kuendelezwa siku nzima; bila shaka kudura ya kiungu itakubali kitu hicho kitokee.. Kwa sababu kuruhusiwa kwa dua hiyo kufanyika kwa msisitizo namna hii ni ishara ya kujibiwa kwa dua hiyo. Kwani, Allah huwa hatoi upenyo wa kufanyika kwa msisitizo DUA ambayo hatoikubali.

Kama mtu si mwenye kusisitiza katika jambo fulani, basi nafasi ya dua hiyo kufanikiwa ni ndogo sana.

Temesema kwamba dua ifanywayo katika hali ya SIJIDA, hasa ikiwa baada ya kukiri makosa, huwa ni yenye nguvu ya hali ya juu sana... Kwa nini...?

Katika hali ya SIJIDA, damu huenda kwa wingi kichwani na kwenye ubongo; ubongo hulishwa vizuri sana na oksijeni na vyanzo vingine vya nguvu. Kwa sababu hii basi unapata uwezo wa kurusha mawimbi yenye nguvu sana.

Vile vile katika hali hii ya SIJIDA huwa kunapatikana ukolevu wa mawazo na uelekeo kwa kitendo cha kukiri makosa; hali hii inakuwa kama chombo cha kufanikisha urushwaji wa mawimbi yenye nguvu katika uelekeo wa kitu kinachohitajika.

Jambo muhimu lenye kuipa nguvu na kuifanikisha dua ni kuwa mbali kwa ufahamu wa mtu kutoka katika ukanda wa utawala wa nguvu ya WAHM pindi dua inapofanyika... Na hali hii ni sijida yani hali ambapo wazo la umimi linatoweka. Ndiyo maana Rasulullah (A.S) akashauri DUA ifanyike “hali ya kuwa na uhakika kwamba itakubalika bila shaka wala hofu”.

Nguvu kubwa inayokata athari ya dua ni nguvu za WAHM wa WASIWASI ambazo pia zipo kwa mtu mwenyewe...

Kiwango ambacho WAHM na WASIWASI vimepungua kwa mtu, kinawiana na ufasaha pamoja na uharaka wa kufanikiwa kwa dua ya mtu huyo.

Moja ya sababu muhimu zilizolala katika kukubaliwa kwa dua za watu waliopata yaqiin kwa ALLAH ni udogo waWAHM na WASIWASI walionao. Kwa upande mwingine hakuna shaka kwamba udhihirikaji wa nguvu za kiungu katika maumbile yao, kama matokeo ya matendo waliyofanya pamoja na  upendeleo wa kiungu, pia ni jambo muhimu lililopo katika kufanikiwa  kwa dua zao kwa haraka.

Hali kadhalika katika suala la DUA, MAJINI wanaojulikana kwa sifa ya USHETANI wanakawaida ya kumpandikizia mtu fikira potofu sana kiasi cha kumfanya asiitumie hii silaha yenye nguvu. Pindi unapojisikia kufanya DUA,MAJINI wanaoitwa SHETANI kutokana na sifa ya ushetani, bila kuchelewa wanakupa wasiwasi...

“Kwa nini nifanye dua, litatokea kama lipo kwenye kadari ...”

“Nifanye dua au nisifanye dua lililopangwa ndilo litakuwa, kwa hiyo sina haja ya kufanya DUA.”

Na hivyo basi unaahirisha kufanya DUA, na kujinyima kutumia DUA ambayo ni silaha yenye nguvu kabisa. Mambo unayokuwa umejikosesha unapojinyima DUA kwa kutokufanya DUA, hayaelezeki wala hayafikiriki. Ni kwa sababu hii basi, tazameni Rasulullah (A.S) kashauri nini:

“Ombeni kila kitu kuanzia viatu mpaka majani ya kondoo wenu kutoka kwa Allah...”

“Ombeni fadhila ya Allah, kwani anapenda kuombwa ”.

“Bila shaka Allah anawapenda sana waja wake wanaofanya DUA kwa kusisitiza”.

“Jueni kwamba kufanya DUA katika nyakati ambazo mnahisia ni bahati, kwa sababu hali hiyo ni hali ya wakati wa rehema”

Maana inayoashiriwa na hadithi ya mwisho ni hii ifuatayo:

Ikisemwa, nyakati ambazo mnahisia, inamaanisha kuwa na unyenyekevu wa hali ya juu kutokana na kukusanya mawazo kwa ukamilifu juu ya jambo moja. Basi wakati huu unamaanisha uelekeo wa dhati wa mtu kwa ALLAH. Uelekeo wa namna hii, kwa ubongo kujielekeza katika lengo moja tu, unazaa ufungukaji wa nguvu za kiungu alizonazo mtu...

Jambo muhimu kuliko yote katika kufanikiwa kwa DUA ni kubaki kwa HAQ kama ndiye mwenye kusema hiyo DUA na mwenye kuleta hilo hitaji katika ubongo wa mtu baada ya mtu kujitokomeza mwenyewe. Na hapa inakuwa;

“Anapotaka kItu kIWe, anasema kuwa nacho kInakuwa”

Moja kati ya mambo muhimu saidizi katika DUA ni kuwa mng’ang’anizi juu ya kitu kinachoombwa. Ni makosa makubwa sana kufanya dua juu ya jambo fulani mara mbili-tatu halafu kuacha.

Inabidi uwepo ung’ang’anizi katika jambo linalofanyiwa dua na inabidi kuwa makini kwa kadiri inavyowezekana kwamba kitu kinachoombwa kiwe chenye kulenga maisha yetu ya baada ya kifo na chenye faida. Kwani, tunaweza kujiumiza vibaya kwa kukosea kuomba. Inafanana na umeme, kama ambavyo tunaweza kuutumia kwa manufaa, hali kadhalika  tunaweza kuutumia kujiumiza au hata kujiua wenyewe.

Tumesema kwamba Dua ni njia ya kujitambua kwa nguvu zinazomilikiwa na ALLAH zilizopo katika uwepoji wako, uMIMI wako, NAFSI yako.

Hivyo basi kwa kadiri tunavyoweza kuitumia kwa akili na ufasaha silaha hii, ndivyo hivyo tutaweza kujilinda dhidi ya maadui zetu, kufanikisha matakwa yetu, na zaidi ya hayo kupata yaqiin kwa ALLAH...

Tumezungumzia uzatitiwaji wa ubongo na nguvu za kiungu ndani ya kitabu chetu cha “MTU na SIRI ZAKE”; Kwa kuelezea mfumo wake  tuliandika mwaka 1984 kwamba, hata ikibidi mawimbi ya ubongo wa mtu yanaweza kusababisha silaha zisifanye kazi.

Tazameni namna ambavyo hata Warusi, ambao si waumini, wanautumia ubongo hii leo:

Tusome kwa makini habari ifuatayo iliyoandikwa katika Gazeti la Sabah la tarehe 11 Juni 1991 ukurasa wa 8.

“VITA VYA BAADAE VITAKUWA VYA TELEPATHY

Mwanasayansi maarufu wa umoja wa Sovieti Vlail Kaznatcheev, ameeleza kwamba ubongo wa binadamu utakuwa unaweza kuathiri vita kwa njia ya Telepathy. Prof. Kaznatcheev, anaendeleza utafiti ndani ya maabara maalumu iliyoundwa ndani ya Novossibirsk Akademy ambayo ni taasisi iliyokusanya watu wenye vipaji vya hali ya juu.

Profesa Vlail  Kaznatcheev ambaye pia ni mmoja wa wanachama wa Taasisi ya sayansi ya Sovieti mjini Mosko, ameeleza kwamba ubongo wa mtu unaweza kuathiri watu, mawazo na vifaa vya elektronik vilivyopo hata mahali ambapo ni mbali sana kutoka mahali ulipo mwili.

Kaznatcheev ambaye ameingia kwenye utafiti wa hali ya juu ili kuthibitisha maoni yake haya ambayo yanachukuliwa kama maneno ya mwendawazimu na watu wengi, amevutia wengi nchini kwake huko umoja wa Sovieti. Serekali ambayo imempa wasaidizi pamoja na maabara yenye vifaa maalumu ndani ya taasisi iliyolea watu wenye vipaji vya hali ya juu, inamatarajio makubwa kutoka katika utafiti wa Kaznatcheev.

Ulinzi wa KGB

Sifa kubwa ya utafiti wa Kaznatcheev ni kujaribu kutumia nguvu ya ubongo wa mtu kwa njia ya Telepathykama silaha. Kwa mtazamo wake, kwa kutumia nguvu ya kufikiria peke yake inawezekana kuharibu mitambo ya kompyuta , rada za viwanja vya ndege, hata silaha zilizotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Serekali ambayo inafuatilia kwa karibu utafiti huu imeunda kikosi cha mashushushu kabambe wa KGB kumlinda Kaznatcheev asitekwe na CIA. Mwanasayansi huyu mashuhuri anafafanua maoni yake kwa mifano rahisi kabisa:

“Kama kompyuta unayotumia imeharibika ghafla, usikimbilie kuwalaumu watengenezaji . Stress uliyonayo au hasira zako, hata kidogo wakati unaitumia, inaweza kuathiri mitambo. Kwa sababu Ubongo wa mtu wa kawaida tu, unanguvu ya juu zaidi ya kompyuta na mara nyingine mtu anaweza kuzitumia nguvu za asili alizo nazo bila kujijua”

Kwa mujibu wa Kaznatcheev, iwapo mtu amemuwaza sana mtu mwingine ambaye hajaonana nae muda mrefu, na mara akapata simu au barua kutoka kwake, asidhani kwamba hiyo ni bahati. Hii imesababishwa na kumuathiri mtu anayemfikiria kwa mawazo aliyonayo.

Kaznatcheev, kwa mara ya mwisho katika kipindi cha TV alichoshiriki aliuonyesha mmea mmoja uliopo katika maabara yake na kuuonyesha kwa muda mrefu na kuwapa watazamaji muda wa saa moja wafikirie ukuwaji wa mmea huu. Matokeo yake kweli yalikuwa ya kustaajabisha, ndani ya muda mfupi, mmea ulionyesha ukuwaji ya hali ya juu.

Kwa upande mwingine utafiti wa Kaznatcheev unalenga katika kuivumbua hali isiyo na mpaka ya nguvu ya mawazo. Kaznatcheev ambaye anaendelea na utafiti wake wenye lengo la kufika kwenye ufahamu wa ndani (subconscious) wa mtu kwa kuunganisha sayansi na parasaikolojia, amesema kwamba uvumbuzi wake utazaa matokeo muhimu sana kwa ajili ya kufadhaisha mitambo ya maadui; na kwamba pamoja na hilo yeye sio mwenye kuchochea jambo hili litumike kama silaha, bali kama kitu cha kupoza na kuzuia vita.” Ni kwa sababu hii basi, DUA inaweza kuelezwa kuwa ndiyo nguvu ya hali ya juu kabisa aliyotunukiwa mtu.