Ufunguo

Rafiki yangu fahamu kwamba kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vyenye thamani ulivyowahi kupewa katika maisha yako.

 

Kitabu hiki ni wito kutoka kwa RAB wako; ni ufunuo maalum! Bila kujali asili yako;kazi yako ; shughuli zako; wala dini unayofuata, jua kwamba RAB wako anakusubiri na mlango wake uko wazi kabisa kukupokea.

Usishangae ukauliza mlango wa RAB wako uko wapi; mlongo “HUO” upo kwako; kwenye moyo wako! Nyuma ya mlango unaofunguka kutoka kwako kuja kwako!...

Mlango huu ni mlango wa DUA na DHIKIRI!... Ni mlango ufungukao kutoka moyoni mwako kuelekea kwa RAB wako.

Ni mlango wa HAJA na kumuelekea RAB wako!..

Achana na MUNGU unayemdhania kuwepo Mawinguni na kando yako; Muelekee ALLAH asiye na mwisho  wala mpaka; Tambua kwamba YEYE yupo kila mahali katika kila chembe; na jitahidi KUMTAFUTA ndani ya moyo wako!..

Kisha taka kutoka KWAKE chochote utakacho!.. Mwenza, kazi, lishe;Ukipenda Mola, ukipenda shifa!...

Fahamu kwamba kitu pekee kitakachokufikisha kwenye haja yako ni DUA na DHIKIRI.

Rafiki yangu jua kwamba ALLAH ambaye yupo katika kila chembe kwa sifa zake zote; na ambaye hakuna kilichopo isipokuwa yeye, ATAKUJIBU KUTOKA KWAKO KUJA KWAKO!

Ujue kwamba WEWE ni “KHALIFA” katika ardhi!... Je unahabari kuhusu nguvu kubwa zilizowekwa katika UBONGO WAKO kama KHALIFA? ...

Je unahabari kwamba unaweza ukaufanyisha kazi mfumo ulio ndani yako kwa kutumia DUA na DHIKIRI, na kwa kutumia UBONGO wako wenye sifa za ajabu?

Je unaujua mfumo wa dua uliozawadiwa kwako kama “SILAHA YENYE NGUVU KABISA”?

Mafukara, wanyonge na watu wengine wengi, kwa kutumia DUA na DHIKIRI, wamewaangamiza WATAWALA wengi MADHALIMU!.

Kuna masikini wengi wamepata utajiri mkubwa kwa kutumia DUA na DHIKIRI!...

Wapo wengi wenye matatizo, dhiki, maradhi, mihangaiko na mateso wamepata uokovu na afueni kwa kutumia DUA na DHIKIRI!...

Rafiki yangu fahamu kwamba...

UNACHO kifaa ambacho ni silaha yenye nguvu kuliko zote duniani.

Kwa kujifunza namna ya kuitumia silaha hii yenye nguvu kabisa KATIKA UBONGO WAKO, KATIKA MOYO WAKO unaweza ukafikia mazuri na mema yote ya, hii dunia unayoishi na maisha ya baada ya kifo!..

Hali kadhalika unaweza ukaamua kutoutumia mfumo huu wa DUA na DHIKIRI, ukauacha upate kutu na kuutelekeza, kwa kufanya hivyo ni wewe pia ndiye utakayebeba adhabu yake milele!...

Huu ni mfumo ambao wewe umepewa bure!.. Ni zawadi!..

Humuhitaji mtu yeyote kwa ajili ya DUA na DHIKIRI  na wala huna ulazima kumtumia mtu kama wakili!..

Ukitaka tumia kitabu hiki; ukitaka elekea kwa namna unayoipenda mwenyewe!.. Lakini hakikisha unajifunza namna ya kutumia kifaa hiki chenye thamani kuliko vyote duniani cha DUA na DHIKIRI..

Utaona namna dunia yako itakavyopendeza.

As Sayyid Ahmed HULÛSİ