Kwa Nini Dua?

Rasulullah Muhammad Mustafa alayhissalaam anasema “DUA NI SILAHA YA MUUMINI”. Halafu anafanya ufafanuzi mwingine kuhusu “DUA” kama ifuatavyo:

“DUA NI KIINI CHA IBADA”
Tujikumbushe aya ifuatayo baada ya hadithi hii:
NIMEWAUMBA MAJINI NA WATU ILI WANITUMIKIE 
Kwa maana rahisi kabisa utumwani dua na dhikiri!.
Kwa maana pana utumwa ni ufanikishaji wa kiumbe wa lengo la uwepoji wake...

Hivi tukifanya dua itakubalika?..
Kama mtumwa wangu atanyanyua mikono na kufanya dua, naona haya kuirudisha mikono yake ikiwa mitupu.
Naam, hii ni Hadithi Qudsi... Hadith Qudsi  nyingine juu ya jambo hili inasema:

Ewe mwanadamu, dua hutoka kwako jibu hutoka kwangu; istighfar hutoka kwako na kusamehe hutoka kwangu; toba hutoka kwako kukubali hutoka kwangu; shukurani hutoka kwako, kutoa kwa wingi  hutoka kwangu; subira hutoka kwako, msaada hutoka kwangu... Kipi umetaka sikukupa...
Ifuatayo ni aya inayosherehesha hadithi Qudsi hiyo:
FANYENI DUA KWANGU, NIJIBU
Kuna hadithi Qudsi nyingine yenye kufafanua suala hili:

Mimi nipo kwa mujibu wa dhana ya mja wangu. Basi afikirie atakavyo!..

Yani, mnapofanya dua, kama mkifikiria kwamba dua hiyo itakubalika basi mfahamu kwamba mnachotaka kitatokea!..

Kwa mlengo huu, mmoja wa mawalii wa ALLAH wa daraja la juu Imam Rabbani Ahmed Faruk Serhendiamesema hivi:

Kutaka kitu inamaanisha kukipata kitu hicho; Kwani Allah taala hamuachi mja afanye dua ambayo hatoikubali.

Kimsingi, tutakapotaka kitu kwa namna ya kufanya dua, inatakiwa tukumbuke aya ifuatayo:
“ALLAH ASIPOTAKA NINYI HAMUWEZI KUTAKA”

Suala ni kwamba, ombi litokalo kwako limetoka kwa sababu Allah kataka!.. Kama Allah angekuwa hakutaka hata ninyi msingeweza kutaka.

Kitu kilicho rahisi, cha bure na chenye athari kabisa ni DUA. Ni kwa sababu hii basi DUA imeitwa “silaha ya muumini

Ni namna gani DUA inakuwa silaha ...

Ili kuweza kuelewa hili inabidi kubobea katika tasawwuf...

Mtu kwa uhakika wake ameumbwa kwa sifa za kusudio la jina ALLAH, yupo thabiti na katika hali ya kudumu kwa kutegemea uwepoji WAKE...

Yu hai, anaishi kwa sifa ya UHAI inayokusudiwa na jina la ALLAH la “HAYY”...

Ni mwenye elimu na ujuzi akipanga maisha yake kwa sifa ya ELIMU kama inavyokusudiwa na jina la ALLAH la “ALIM”...

Na ni mwenye kufanya matakwa yake yafanikiwe kwa jina la ALLAH la “MURID”...

Hivyo basi mtu anapata atakayo na kuondokewa na hofu ya anavyoviogopa kwa kiwango kinachowiana na alivyo kadiriwa kudhihirisha maana za majina haya ambayo yapo katika uwepoji wake...

*  *  *

Dua ni nini?
Je niombi kwa Mungu aliye kando/mbele yako?..

Ama ni ombi la kubainisha nguvu ya ALLAH aliye katika kiini cha uwepoji wako, katika namna zote za uwepo wako, ambaye uwepoji wako unamtegemea?..

DUA, si kingine zaidi ya mbinu ya kudhihirisha nguvu za kiungu zilizopo katika uwepoji wa mtu!..

Ni kwa sababu hii, mtu akifanya DUA kwa dhati, ataona yanafanikiwa yale yaliyokuwa yakionekana hayawi.

Ndiyo maana basi, silaha ya mtu yenye nguvu kabisa ni DUA ...

Kama tunataka kupata matokeo mazuri ya DUA, kwanza inabidi tuyape umuhimu mambo kadhaa kuhusu namna ya kufanya dua, mahali pa kufanyia dua, na wakati wa kufanya dua.