Kubainika Kwa Ukhalifa Wa Mtu

Lengo la uwepoji wa Mtu katika ardhi ni kuufanikisha kwa dhati UKHALIFA...

Kuutumia ipasavyo UKHALIFA kunawezekana pale mtu atakapouelewa undani wake yeye mwenyewe pamoja na asili yake; kisha akahisi na kufanikisha yale yote yanayoambatana na UKHALIFA.

Njia ambayo mtu ataitumia kuufanikisha UKHALIFA  ni kujikwamua na kujitakasa kutokana na masharti ya mazingira ya alipozaliwa pamoja na kuacha kutuhumu watu kwa mitazamo ya kidesturi, kisha kujitahidi kujipaMWENENDO WA ALLAH.

Hautojulikana MWENENDO WA ALLAH bila kufahamu ipasavyo LINALOKUSUDIWA NA JINA ALLAH!

Iwapo halitofahamika hili, basi mtu atatengeneza kichwani kwake kiumbe CHA KUKIPAPATIKIA na kukipa jina la ALLAH; Kisha akakipa sifa na nyadhifa mbalimbali kufuatana na shinikizo la mazingira yanayomzunguka, hisia zake  pamoja na desturi ya jamii yake. Mtu huyu ataondoka kutoka duniani akiwa mwenye KUJILIWAZA kwa kujikagua na kujirekebisha kwa kadiri atakavyoweza  kwa mujibu wa huyo MUNGU aliyemtengeneza kichwani mwake.

Elimu ni CHOMBO cha kumuongoza mtu kufanya analopaswa kulifanya!...

Kuufanikisha UKHALIFA ndiyo lengo la uwepoji wa mtu!...

Yaani, lengo pekee la Mtu ambaye ameumbwa awe KHALIFA ni kuvishinda vipangamizi vyote na hivyo kufanikisha UKHALIFA wake.

Kama mtu utashindwa kuondoa katika ufahamu wako, na kujikwamua na yote ambayo kesho utalazimika kuyaacha, hutoweza kukipata kitambulisho chako cha kweli.

Wakati huu tulionao MAMBO YA TARIQA hayapo tena. Yaani kwa maana yake ya dhati, ule uhusiano kati ya SHEIKH na DARWESHI umefika mwisho; Ule uhusiano wa MLEZI na MLELEWA umekwisha toweka!...

Mfano wa mahusiano haya ni kama ule wa YUNUS na TAPTUK!... YUNUS Ndani la baraza la TAPTUK, aliloingia akiwa na miaka ishirini, anakandwa ipaswavyo; anafunzwa namna ya kukaa mpaka kusimama; kula mpaka kunywa; maneno anayotakiwa kuyasema mpaka namna ya kufikiria; kisha anaruhusiwa kurudi mtaani kufanyia kazi aliyojifunza akiwa na miaka miaka sitini...

Jambo hili haliwezekani kwa wakati huu tulionao.

Hutoweza kumpata mtu wa kukusimamia kukurekebisha na kukuongoza kila sekunde!...

Jitakaseni na kujikwamua kutokana na mambo ambayo asili yake ni ndoto!..

Mtu hafunzwi tabia kwa kunyooshewa mkono kutoka mbali!..

Elimu inaweza kuruka kutoka mbali, China kwa mfano; Elimu hii inanaswa na ubongo wowote wenye uwezo wa kupokea elimu hiyo, na kufanyiwa kazi. Lakini mwenendo wako na mapungufu yote ya tabia hayarekebishiki kutoka mbali. Hili ni jambo unaloweza kulifanikisha wewe mwenyewe kutegemeana na kiwango cha elimu yako.

Uwezekano wa kurekebishika kwa hisia, tabia na mtazamo wako kwa msukumo unaotoka mbali ni ndoto ya machana!

Mfumo huu ambao tupo ndani yake ni kazi ya sanaa ya MWENENDO WA ALLAH!...

Quran ni kitabu tulichopewa ili tuweze kuutambua huu mfumo wa ALLAH ambao tunaishi ndani yake...

Kama kwa namna yeyeto ile UELEWO wetu wa Quran hauwiani na MTAZAMO  wetu wa huu mfumo basi inamaanisha kwamba bado hatujai-SOMA Quran!

Quran inapoSOMEKA mfumo unabainika na hivyo kupelekea kubainika kwa MWENENDO WA ALLAH...

Daraja la UKHALIFA WAKO linawiana na kiwango chako cha kuuvaa MWENENDO WA ALLAH pamoja na uwezo wako wa kuchambua mambo kwa mujibu wa mtazamo huo.

Hakuna fimbo itayotoka MAWINGUNI  kuja kukufanya uwe KHALIFA au WALII; kwani haya ni majina ya mwenendo na mtazamo katika maisha...

Kama wewe huna mwenendo au Mtazamo huu basi hautoweza kubadili sifa uliyonayo hata kama ukijivisha kitambulisho chenye maandishi ya dhahabu cha kukuonyesha wewe unasifa hizo.

Nawashauri “MSIZIDHULUMU NAFSI ZENU” kwa kujilaghai wenyewe na matarajio ndoto!.

Kinachokufikiaeni ni elimu ambayo ndiyo Shifaa (Muombezi).

Kwa mujibu wa elimu hiyo mtachonga maisha na kujitahidi kujikomaza...

Mtu mwenye Akili ni yule mwenye kufanya jitihada kujikomaza(Kujiendeleza)... Hapotezi muda wake bure kwa kuhangaika na wanaomzunguka katika mambo yasiyo muhimu!.. Kumbuka kwamba ni Faradhi kusambaza unayoyajua!... Tabligh ni FARADHI... Hali kadhalika ni faradhi kutowalazimisha watu katika jambo lolote lile baada ya kuwafahamisha.

Hivyo basi jukumu la kila mmoja wetu ni kunufaika na elimu kwa moyo safi bila kufungwa na ndoto za mchana; Kuwakubali watu kama marafiki tuu na kuzingatia ushauri wao bila kuwafanya masanamu ya kuyapapatikia; Kukubali ukweli wa kwamba lolote litakalotusibu ni matokeo ya tuliyoyafanya, na hivyo basi kujitahidi kuchonga njia zetu wenyewe bila kuwa na ndoto ya kuwatwika wengine mizigo yetu...

ALLAH awe ameturahisishia kufanikisha yote kwa mujibu wa elimu!.

AHMED HULUSI
14.6.1998
New Jersey USA
Kutoka katika kitabu: WITO WA MFUMO