Elewenı "Islam" Na Sıo Uıslam

Siku hizi kuna waliopewa ufahamu na wanaoonekana kana kwamba wamepewa ufahamu!.

Kunawasomi na wanaoonekana wasomi!.

Kunawashinikizaji na wanaotaka kushinikizwa!

Kuna “ISLAM”; Kuna “Uislam”!.

Waliopewa ufahamu ni wale wenye kupata ukweli na kuuelewa baada ya kuchanganua nyaraka kwa mtazamo ulio huru!. Wanaoonekana wamepewa ufahamu ni wale wenye kujaribu kukusanya michango kwa kutumia yale waliyoyaelewa kutoka kwa wenye ufahamu na kuuza kwa wale wanaowazunguka!.

Wapo wasomi duniani... Wanaojitahidi kuchonga maisha yao kwa akili kwa kutumia fikira za kisayansi!  Wapo wanaoonekana wasomi; wanaoiga wasomi waliowavutia. wanatamani kuvaa, kula, kunywa na kuzungumza kama wao!.. 

Ni madini hewa yanayong’aa vichochoroni. Ung’avu wao unawasisimua hao wavichochoroni!.. Lakini hawajapata kuona; hawajui  tofauti kati ya kito cha kweli na cha bandia. Kwa hiyo hawa ndio walengwa wa hayo madini bandia! Na wako radhi kutoa vingi mno ili  wafanane nayo, lakini hawatoweza hata kidogo!

Wapo wanaopenda kushinikiza watu kwa sababu ya maumbile na uweza wao.. wanawaongoza na kuwatawala watu; wanafanya hivi katika uelekeo wa kupata faida kimali au kiroho!. Wanatengeneza vikundi kwa ajili ya kuvitawala, kuvipa amri na kukidhi hamu yao ya ukamanda ambao wameshindwa kuufanikisha. Kwa upande mwingine wapo wale wanaopenda kushinikizwa nakufanya utumishi ; wapo ambao kujiamini kwao kunategemea hili; unyonge wao wameamua kuuonyesha katika namna hii!.

Hali ni hii kila pahala duniani!

Ukweli ni kwamba Allah amemuumba mtu kama kiumbe chenye hadhi ya juu kuliko vyote, amejaalia awe Khalifa katika ardhi; Lakini nani anajali!.

Ndiyo! hawa wanaoonekana wasomi wakishirikiana na wanaoonekana wamepewa ufahamu wanaujadili uislam ambao hauna mantiki wala hauwiani na sayansi; Kwa kusisitiza hali ya kubaki nyuma ya watu wanaoufuata “UISLAMU” wanadhani kwamba wanakosoa “DINI YA ISLAM” !.

Watu hawa kutokana na kutojua, hawafahamu tofauti kati ya “DINI YA ISLAM” na “UISLAM”, na kwamba swala la dini haligusiki bila kufahamu tofauti hii!

Kwa kuchukua mawazo yenye thamani ya madini bandia kana kwamba ndio wazo la msingi wa dini ya ISLAM wanaacha madini yenyewe kutokana na kuta kujua.

Wanakosa jinsi ya kufanya wenye kuhitaji kufunzwa; kwani vyanzo vya kujifunza walivyonavyo ni uzushi wa wakandamizaji na maneno ya wapambe wao!...

Wanaiangalia Dini ya ISLAM kana kwamba ndiyo uislam wa wale watu wenye kuchukulia MAULIDI kama ibada; wanaosherehekea Nyisiku zenye thamani; Wanaodhani kwamba sharti la kwanza la kuwa muislam ni mwanamke kujifunika kichwa; wanaodhani kwamba Swala na funga vimewekwa ili kumfurahisha mungu wa mawinguni wa wapapatikiaji wa mungu wa mawinguni!.

Hawaelewi kwamba maulidi ni shairi liliandikwa na Suleyman Chelebi, na kwamba haina uhusiano wowote na ibada zilizotajwa na Quran. Hawajabaini kwamba nyisiku za Miraj, 15 Shabani, Qadir si kwa ajili ya kuwasha mishumaa kwa maiti wetu, utaratibu ambao hauna uhusiano na Dini, bali ni nyisiku zenye masaa yenye thamani... Hata hawajasikia ya kwamba hakuna sikukuu ya kuchinja na ya peremende bali kuna ufanikishwaji wa sikukuu za FITR na HAJ. Hawajaelewa kwamba Swala, Funga na Hija zinazoelezwa na Quran si kwa ajili ya kumfurahisha Mungu wa Mawinguni bali ni kwa ajili ya kuokoa maisha yao ya baadae!

“DINI YA ISLAM” ni mfumo na utaratiibu katika enzi ya Allah ulio juu ya wazo la muda!. Ni chanzo, ni kiini, haibadiliki na wakati... Huu ndio ufafanuzi wa Quran!.

“UISLAM” ni uchanganuzi wa watu wa dini ya ISLAM kutegemeana na uwezo wao, mashinikizo, mila na desturi za mazingira yao ndani ya mipaka iliyowekwa na watawala wao.

Umefika wakati wa kuelewa kwamba machanganuzi hayadhibiti Dini ya Islam!.. Jitahidini kubaini kiini!.

Achaneni na UISLAM na mtazame Dini ya Islam!

AHMED HULUSI