“Qadir” Ya Mungu Itokayo Mawinguni

Ndani ya ufahamu wa dini unaoegemea kwenye wazo la Mungu, unadhaniwa kuwepo usiku ufuatao ambao wanauita “Usiku wa Qadir”...

Mungu aliye mkubwa, ameandaa neema kwa watumwa wake aliowachagua katika ardhi!.. kwa ajili ya kuwalipa wale wanaompapatikia sana. Neema hiyo kubwa ameiita “QADIR”...

Malaika wanaoileta (!) hiyo neema, wanashuka kwenye kitongoji wanachoishi waislamu ndani ya usiku mtakatifu wa maadhimisho, - Kwani, huangamia wakiona mwanga; Kwa mfano wa vitamini C iliyopata mwanga!..

Ndiyo hiyo “Qadir isiyouona mchana”(!)  ambayo ni kitu (!) kilicho bora kuliko upapatikiaji wa miezi 1000, yani miaka 83.

Kila mwaka tarehe 27 mwezi wa Ramadhani, Malaika wakiwa  na amri ya Mungu Mkubwa, hushuka umbali wa miaka mingi kuelekea Duniani kwa kasi, huku wakichapa mabawa yao, na kuanza kuwatafuta nyumba baada ya nyumba watumwa wanaofanya upapatikiaji katika eneo ambalo ni usiku wakati huo.

Wakati huo basi wale wote wanaoishi mahali ambapo ni mchana hawaambulii chochote!

Kwa mujibu wa vigezo walivyonavyo mkononi, kama watampata mpapatikiaji muadilifu, bila kuchelewa humuuliza mola wao, “Je huyu tumpe QADIR?” ... Kama Mungu ataidhinisha, bila kuchelewa mtumwa huyo hupewa “Qadir”. Shughuli hii ya utafutaji nyumba baada ya nyumba  au, ya kugawa hii “Qadir” inaendelea hivyo mpaka jua linapochomoza.

Haijulikani idadi ya watu watakaopewa “Qadir” usiku huo!. Haijulikani vile vile kinachobadilika kwa watu wanaopewa “Qadir” !...  Mionzi ya mchana inapooneka malaika pamoja na roho, bila kuchelewa, hurudi kwenye viota vyao vilivyopo kando ya Mungu mkubwa!.

Katika kipindi hicho, watumwa walioamini wanazunguka msikiti baada ya msikiti, wakitarajia kubahatisha zawadi hii katika msikiti mmoja wapo!.

...

Kwa mujibu wa ufahamu wa “DINI” unaoegemea kwa Rasulu wa Allah Muhammad Mustafa aleyhissalaam, kwa mujibu wa watu tunaowaita Ahlullah ufafanuzi au uchanganuzi wa kinachoelezwa kama usiku wa “Qadr” ni huu ufuatao:

Tumeubainisha katika ufahamu wa mtu “Mjumuiko wa siri” unaokusudiwa na jina Qur’an pamoja na “Asili yake iliyopo katika kiini chake” (Anzalna HU), ndani ya kipindi ambacho mtu huyo anaushuhudia u”potea”ji (Layl) wa uwepoji wake. Yakumbukwe maelezo ya kwamba “Qur’an na Mtu ni mapacha”.

Je unajua ni nini hii asili au siri (Qadr)?
Giza la u”potea”ji (Usiku) ambalo ndani yake inafanikiwa hali ya Qadr, ni lenye heri kuliko yanayoweza kufanikishwa katika kipindi cha miezi 1000 (Muda wa uhai wa mtu wa karibu miaka 80).

Malaika(nguvu za kimalaika – mabawa yanakusudia idadi 2-3-4 ya uelekeo wa ufanyaji kazi wa nguvu hizi) naroho(maana ya asili, u’yeye’ “HU” wa uwepoji wao) , hubainika katika ufahamu wa mtu kulingana na idhini(uwanja wa kufanikisha mambo - uwezo) ya Rabb wa mtu (muunganiko wa majina (Asma) – muunganiko wa majina ya Allah yanayofanya uwepoji wake) huyo; na hivyo basi katika muda huo, kwa kujumuisha na hisia ya u”potea”ji wake, atamuhisi na kumbaini “ALLAH” ambaye yupo kwa ukamilifu! Mtu huyu atakuwa ndani ya u“Salaama” kutokana na kila aina ya hukumu!.

Hali hii huendelea mpaka hisia na fikira za uwepoji, utu zitakapozidi uzito (anaporudi ALFAJRI).

Uwezo huu utafuteni usiku wowote katika mwaka, yani, katika kila hali ambapo mnaweza kuuhisi u”potea”ji wenu ndani ya enzi ya kusudio la jina ALLAH!... imedokezwa, “Utafuteni usiku wa Qadr ndani ya kila usiku katika mwaka.”... 

Imedokezwa, “Utafuteni ndani ya Ramadhani” ...jaribuni kuipata hali hii katika kipindi ambacho mnafanya jitihada za kujikwamua kutoka kwenye utu na kuihisi asili yenu kwa funga inayofanikishwa kwa maana ya kweli!

Imedokezwa, “Utafuteni siku za mwisho za mwezi wa Ramadhani”... Utafuteni katika hatua za mwisho za utakaso wa kiroho unaopatikana kama matokeo ya ufanikishaji wa funga ambayo si ya kuiga bali iliyo ya uhakika!.

Sasa ngoja nijaribu kuelezea kwa ujumla yale tuliyoyaelewa kutoka katika maelezo ya ufananishaji kwa kutumia ishara ndani ya “Suratul Qadr”:

Kuna muda (Muda wa Qadr) ambao ni wenye heri zaidi kuliko anayoyafanikisha mtu katika kipindi cha uhai wake; Ndani ya huu ufunuo au mlipuko wa muda mchache katika ufahamu, taharifa kuhusu asili yake zinashuka (Tanazzul), yani zinafunguka “kutoka katika kiini chake kuelekea kwenye ufahamu wake” !. Hii ni asili ya (uhakika wa) u’yeye’ wa “HU”.

Uhakika huu, kwa mujibu wa kanuni inayosema, “Mtu ni siri ya Qur’an; Qur’an ni siri ya Mtu” , unafunguka kutoka ndani ya mtu!.

Wakati gani?

Mtu, baada ya kuanza kwa kujiuliza mimi ni nani, kumuamini Rasulu wa Allah Muhammad alayhissalaam, kuelewa aliyoyaleta na kwa kujikwamua(kujitakasa) kutokana na wazo la Mungu, kuelewa kusudio la jina “ALLAH”, kimsingi kwa kiwango kilichoelezwa ndani ya Sura ya “Ihlas” ... anapotumbukia katika kiza la kuuhisi u’potea’ji wake, katika enzi ya aitwaye kwa jina pekee la ALLAH, kutoka katika uwepoji wa utu wake, yani mwangaza wa mchana; na vyote vilivyopo, kupoteza uwepoji wake katika uonaji wa mtu huyo...

Ndani ya muda anapohisi na kubaini kwamba sifa za majina ya Allah ambazo ni kiini chake (uhakika wake) ndizo zinazofanya uwepoji wake, atapata udhahiri na atafahamu kwamba ROHO, yani maana ya majina haya pamoja na Malaika, yani nguvu za majina haya ni zenye kudhihirika katika maumbile yake kila wakati!..Kulihisi na kulibaini hili ndiyo hali ya “QADR”.

Ndani ya muda huo hatobaki mwenyewe, wala kachembe kutoka katika vionekanavyo vipo...

Atashuhudia ukweli unaoelezwa kwamba, “Je umiliki ni wa nani ndani ya muda huu (Yawm)?” “Lillahil wahidil Qahhar (Ni wa Allah ambaye ni Vahid na Qahhar)”!. Atai”SOMA” “Ash’hadu...”!.. Mwenye kutazama anakuwa yeye mwenyewe!

Hali hii, inaendelea kwa huyo mtu hadi atakapojifahamu tena katika ukanda wa kiutu(Alfajri). Hivyo basi anakuwa miongoni mwa wale waliofanikiwa kuubaini uhakika wa uwepoji wao na baada ya hapo anaanza kuzi”SOMA” siri za Qur’an na anakuwa ni mwenye kusubiri mauti ( badilisho lake la ukanda – dimension) na wakati huo huo anakuwa ni mwenye kuendelea na “UTUMWA – UJA ” wake katika namna inayowiana na lengo la kuumbwa kwake.

Kwa nini tumeliandika hili?...

Nimeandikia ili nichange nanyi ukweli wa kwamba,“Kitabu” kinachoelezwa kama “Kitabu cha Amri za Mungu”, kwa mtazamo wetu sisi kinabeba maana ya “KITABU CHA SIRI” ambacho ni tofauti kabisa; na kwamba bila kujifunza u”SOMA”ji wake, kuna mambo mengi yatakosekana...

Huu ni mfano mmoja ... Ukianza na “MI’RAJ” kuna mifano kama hiyo mingi tuu ambayo inabidi ifafanuliwe, ndani ya HICHO Kitabu ambacho ni Usemaji (Qalam) wa Allah!...

Inasikitisha kwamba hata roho za wengi wetu hazina taharifa yoyote kuhusu haya!!! Bado tunadhani kwamba Qur’an Karim ni kitabu cha historia na amri za mungu!...

Katika uchanganuzi huu naweza kuwa niko sahihi, au nimepotoka!. Lakini hivi ndivyo tulivyosoma kutoka katika vitabu vya watu tunaowaita Ahlullah...

Kama tuko sahihi katika uchanganuzi huu; wale ambao anashindwa kuufanyia kazi mtazamo huu wafikirie wenyewe ni mambo yapi zaidi wanayakosa!.

Kama tumepotoka; basi tutaangamia vibaya sana katika mikono ya huyo Mungu aliyekaa pahali fulani huko juu, ambaye mara moja kwa mwaka anawatuma malaika pamoja na roho duniani katika kiza la usiku!..

AHMED HULUSI
2 September 2005
(Imetafsiriwa kutoka kwenye lugha ya Kituruki)